Vilio huku na huku, kila mmoja ni Korona
Nyoyo mejawa shauri,wanadamu twasonona
Tunakufa kama kuku, uchumi kwama kina
Waziona atharizo? Watutesa sema mbona
Dada zetu taabani, kisa korona nyanjani
Mimba Tele hesabuni, visa vipya kupandani
Vidume ni wani wani, kisawe wadanganywani
Waziona atharizo? Watutesa sema mbona
Wenda pasi ufahamu, wa njia zilo salama
Ila swezi walimu, mana Hawaii njema
Kupityawe wadhulumu, ona yanowaandama
Waziona atharizo? watutesa sema mbona
Serikali mashakani, wakumnusuru nani?
Usalama mipakani? Ama vijana nyumbani?
Wagonjwa sipitalini, ama wewe maluuni?
Waziona atharizo? watutesa sema mbona
Tamati tama sikatai, ingawa wajona bingwa
Sanitaza kwa wakati, naamini utashindwa
Barakoa ni shuruti, umbali ulishapangwa
Waziona atharizo? Watutesa sema mbona
Chairman, Mombasa County, Teddy Ruwa
2 thoughts on “Changamoto za Corona”
💪💪💪
Nzuri